Madiwani wailaumu MUWASA uhaba wa maji Katavi




Na Adelina Kapaya,katavi.

Baadhi ya kata  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi kumekua na uhaba wa Maji kutokana na miradi inayofanywa na mamlaka ya maji MUWASA kushindwa kukamilika.

Madiwani wakata  hizo wameonekana kutofurahishwa na uwajibikaji wa mamlaka hio na kuomba muhandisi wa mamlaka ya maji MUWASA Zakalia Nyanda kutoa ufafanuzi wa kina kwa visima vilivyochimbwa bila kuwekewa pampu kwa muda murefu.

Wamesema kuwa wamekua wakimfuata muhandisi  wa mamlaka hio na kuwapa majibu yasiyolidhisha hali inayopelekea kutomuamini na kuona  ni udanganyifu kwa Yale anayowambia

Akijibu maswali ya madiwani  Nyanda amesema mamlaka imeshindwa kumalizia kuweka pampu kwenye visima vilivyochimbwa kwa sababu fedha na vifaa vilivyokuepo vilitumika kurekebisha mabomba yaliyohalibiwa na TARURA wakati wakitengeneza barabara.

Amesema kuwa mabomba hayo yalipasuliwa kutokana na maandalizi ya ujio wa Rais  John Magufuli mkoa wa katavi wakati TARURA wakirekebisha barabara.

Mpaka sasa TARURA ina  deni ya million 30 kutokana na uharibifu walioufanya lakini mpaka sasa hawajaripa kiasi chichote cha fedha kwenye mamlaka ya maji MUWASA hali inayopelekea baadhi ya miradi kushindwa kumalizika.

Baada ya majibu hayo mwenyekiti wa Halmashauri Deodatus Kangu amemshauri Muhandisi Nyanda kushirikiana na mamlaka ya maji MUWASA kuhakikisha maji yanapatikana kama Rais alivyoagiza akiwa katika ziara yake.

Takribani visima 13 havijawekewa pampu hivyo wakazi wa Manispaa ya  Mpanda hususani Kata ya Mpanda Hotel na Makanyagio hukumbwa na adha ya uhaba  wa maji kwa muda murefu.