Mbunge aliyesema Wahudumu wa kike ATCL hawana mvuto aomba radhi


Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM),  Husna Mwilima ameomba radhi kwa kauli aliyoitoa bungeni Novemba 7, 2019 akisema wahudumu wa Shirika la Ndege la ATCL hawana mvuto hivyo kupelekea kutokuwa na hamasa kwa wateja.

"Nilitoa ile kauli lengo lilikuwa ni kuboresha Shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuwa ile kauli yangu iliwaboa sana Watanzania hasa wanawake nitumie nafasi hii kuomba radhi Watanzania hasa wanawake wenzangu," amesema Mbunge Mwilima.

Mara baada ya kutoa kauli hiyo, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimpongeza na kusema "Huo ni uungwana."


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items