BREAKING: Mchekeshaji Idris Sultan amuomba radhi Rais Magufuli


Msanii wa vichekesho Idris Sultan amemuomba radhi Rais wa Tanzania, John Magufuli kutokana na kuhariri picha ya kiongozi mkuu huyo wa nchi na kuiweka katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo Dar es Salaam na Waandishi wa Habari, Idris amesema kuwa anafahamu Rais ana haki ya kukereka na kitendo alichokifanya hivyo hana budi kuomba radhi kwa kufanya hivyo.

"Kwa hiyo naomba radhi kwa Rais kama picha yangu imemkera kwa jinsi nilivyomtakia. Nakuomba radhi Mheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama kiongozi wangu wa awamu hii," ameeleza Idris.

Mchekeshaji huyo amesisitiza kuwa lengo lake la kuhariri picha ya Rais Magufuli ilikuwa ni kufurahisha watu na kumtaki Kheri ya siku ya kuzaliwa kwake.

Decemba 2014 Idris Sultan alishinda shindano la Big Brother Africa Hotshot baada ya kutupa karata yake kwa takriban miezi miwili ndani ya jumba hilo lililopo nchini Afrika Kusini na kujipatia kitita cha US Dollar 300,000 ambazo ni zaidi ya Tsh. Milioni 514.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items