Loading...

11/27/2019

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamalizika


Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza Novemba 21 2019, umemalizika hapo jana katika ngazi ya makatibu wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ambapo hii leo utafuatiwa na mkutano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa EAC.

Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya hiyo kuanzia tarehe 27 na 28 November 2019.

Pichani juu ni Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili jambo wakati wa Mkutano wao. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afrika Mashariki - Uganda, Bibi. Edith Mwanje, akifuatiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Tanzania, Dkt. Faraji Mnyepe. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masula ya EAC - Sudani Kusini, Bw. Mou Mou Athian Kuol, Meja Generali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Uganda, Balozi Charles Karamba.

Wengine pichani ni Katibu Mwandamizi, Wizara ya Afrika Mashariki na - Kenya, Dkt. Margaret Mwakima na katibu Mkuu, Office ya Rais Inayohusu masula ya Afrika Mashariki - Burundi, Balozi Jean Rigi.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger