Kocha wa muda wa Yanga, Boniface Mkwasa amebadili ratiba ya muda wa mazoezi ambayo ilikuwa inatumiwa na Zahera Mwinyi.
Afisa Habari wa Mabingwa hao wa Kihistoria, Hassan Bumbuli amesema kwa sasa mazoezi yatakuwa yakifanyika jioni na sio asubuhi.
"Mkwasa amebadili muda wa mazoezi, kuanzia sasa mazoezi yatakuwa yakifanyika jioni. Wakati Zahera Mwinyi akiwa kocha wa Yanga mazoezi yalikuwa yakifanyika asubuhi" amesema Bumbuli.
Katika hatua nyingine Mkwasa pia anataka kupata mchezo wa kirafiki kabla ya kukuta na JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi.
Lengo la mchezo huo ni kutaka kuwaona wachezaji wote kwa sababu alikwenda Mtwara kucheza dhidi ya Ndanda akiwa na wachezaji 20 wengine walibaki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha.

