Watu wapatao 18 wamepoteza maisha yao na wengine 13 kujeruhiwa baada ya basi la abiria kuteleza kutoka kwa barabara na kutubukia kwenye shimo la mita 400 kusini magharibi mwa Nepal.
Afisa mwandamizi wa serikali alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Narapani la Sandhikharka Manispaa ya kusini mwa wilaya ya Arghakhanchi.
Watu 17 walikufa kwenye eneo la tukio na mmoja alikufa hospitalini, Afisa Mkuu wa Arghakhanchi Bijaya Raj Poudel aliliambia shirika la Xinhua.
