Polisi wa Afrika Kusini wawakamata wahamiaji haramu 300


Polisi wa Afrika Kusini wamewakamata wahamiaji haramu 300 mjini Johannesburg. Polisi wamesema kikosi mseto kiliwakamata wahamiaji hao kwenye jengo lenye ghorofa 21 lililovamiwa katika eneo la Hillbrow, mjini Johannesburg.

Hillbrow ni eneo la mji wa Johannesburg linalojulikana zaidi kwa msogamano wa watu, ukosefu wa ajira, umaskini, ukahaba na uhalifu.

Watu hao wamekamatwa wakati polisi wanafanya msako wa watu kuzuia uhalifu na kuweka ulinzi kwa ajili ya kipindi cha sikukuu zijazo.

Msemaji wa Polisi Brigedia Mathapelo Peters amesema kati ya watu 380 waliokamatwa 353 wakiwa ni wanaume na 27 wakiwa ni wanawake, ni raia wa Malawi na Zimbabwe ambao sasa wanachunguza kuhusu ukazi wao.