Rais Trump asema Marekani imeanzisha mazungumzo na Taliban

Rais Donald Trump amesema Marekani imeanzisha mazungumzo na wanamgambo wa Taliban wakati alipofanya ziara ya kushtukiza nchini Afghanistan kusheherekea Siku Kuu ya Kutoa Shukrani na wanajeshi.

Katika ziara fupi kwenye kambi ya Bagram Airflied nje ya mji mkuu Kabul, Trump aliwaandalia wanajeshi chakula cha jioni ambacho kitamaduni kilijumuisha bata mzinga, akapiga picha nao na kutoa hotuba baada ya kukutana na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.

Aliwaambia wanahabari kuwa Taliban wanataka kufikia makubaliano na Marekani inakutana nao ili kuwashinikiza kufikia makubaliano ya kuweka chini silaha.

Karibu wanajeshi 13,000 wa Marekani bado wako nchini Afghanistan, miaka 18 baada ya Marekani kuvamia nchi hiyo baada ya mashambulizi ya Septemba 11.

Trump amesema anataka kupunguza idadi hido hadi 8,600 bila kutoa maelezo zaidi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items