Rais wa FIFA aeleza mipango ya kuinua vilivyo soka la Afrika


Rais wa Shirikisho la soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametoa wazo la kuunda Ligi ya Vilabu barani Afrika na Ujenzi wa Mabilioni ya viwanja vya kandanda.

Infantino ametoa mawazo mawili ambayo yatainua maendeleo ya soka la Afrika, kwanza kuunda Ligi ya Soka la vilabu ambayo itajumuisha vilabu bora Afrika, pili uwekezaji mkubwa wa kujenga na kuboresha viwanja.

 “Nataka kulifikisha soka la Afrika kwenye kilele cha Dunia," asema Infantino.

“Inabidi upate vilabu bora 20 barani Afrika na kuvifanya vicheze katika mashindano ya mfumo wa Ligi Afrika na hiyo Ligi inaweza kuzalisha angalu Dola Milioni 200 ya mapato na kuwaweka katika kumi bora Duniani kwa haraka sana," alisisitiza.

Changamoto ni kuzuia kuondoka kwa wachezaji bora Afrika kwenda katika Ligi zingine Duniani kwa mujibu wa Infantino.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items