https://monetag.com/?ref_id=TTIb Makamishina wa Tume ya Haki za Binadamu atakiwa kuimarisha misingi ya utawala bora | Muungwana BLOG

Makamishina wa Tume ya Haki za Binadamu atakiwa kuimarisha misingi ya utawala bora


 Na Thabit Madai-Zanzibar

Mwenyekiti  wa Tume ya Maadili Zanzibar, Asaa Ahmed Rashid  amewataka Makamishna wa Tume ya haki za binaadamu kuimarisha haki za binaadamu na misingi ya utawala bora kwa kuandaa mpango maalumu wa  kuwaelimisha wananchi ili  kuweza kujua wajibu wa kulinda na kutetea haki zao.

 Akifungua Mafunzo Elekezi kwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali  Suleiman huko katika  Ukumbi wa Hoteli Madinat Al Bahar iliopo Mbweni.

Alisema Makamishna hao wameaminiwa na Serikali kwa  kusimamiana kuimarisha haki za binaadamu na kutoa maamuzi pamoja na kupokea malalamiko yanayowasilishwa na wananchi kwenye Tume  kwa kuzingatia Katiba na Sheria za Nchi.

Alisema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuziingiza haki za binaadamu katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano  ya mwaka 1977 kupita mabadiliko ya tano ya mwaka 1984.

Aidha alisema mwananchi yeyote wa Tanzania ambaye atahisi haki zake za msingi zinakiukwa anayo fursa ya kupeleka malalamiko yake mbele ya Mahakama au vyombo vyengine vilivyoanzishwa kisheria.

"Suala la haki za binaadamu ni jambo la msingi katika nchi  zinazothamini utu, demokrasia na maendeleo ya  jamii  Makamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora waliopata dhamana kusimamia haki", alisema Mwenyekiti huyo .

Naye Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Fatma Muya  alisema  majukumu ya Tume kuzilinda kutetea haki za binaadamu katika Misingi ya Utawala Bora.

Kwa upande wake Kamishna wa haki za binaadamu Zanzibar Khatibu Mwinyichande alisema  kazi  zao ni  kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuwapatia haki zao zinastahiki kwa mujibu wa sheria .

Hivyo Alisema Serikali imeandaa vyombo katika Tume za Haki za binaadamu kwa lengo la kusikilizwa wananchi ambao wanamalalamiko yao na kufanyiwa kazi.