Wafanyakazi wanne kwenye kituo cha Ebola nchini DR Congo wauliwa


Shirika la afya duniani (WHO) limesema mashambulizi mawili yaliyotokea Mashariki mwa DR Congo, yamesababisha vifo vya wafanyakazi wanne wanaoshughulikia mlipuko wa Ebola nchini humo na wengine watano wamejeruhiwa.

WHO imesema mashambulizi hayo yalitokea usiku kwenye kambi ya pamoja ya machimbo ya Biakato na ofisi ya uratibu wa ushughulikiaji wa Ebola huko Mangina, mji mdogo katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Watu waliouawa ni pamoja na mhudumu wa kikundi cha chanjo, madereva wawili na ofisa wa polisi.

Mkurugenzi wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, ugonjwa wa Ebola unaondoka, lakini mashambulizi hayo yanaupa nguvu ugonjwa huo tena, na mat