Mahakama nchini Afrika kusini imekataa leo rufaani iliyowasilishwa na rais wa zamani Jacob Zuma ambao ilitaka kuzuwia kushitakiwa kwake kwa madai ya rushwa kuhusiana na mkataba wa ununuzi wa silaha wenye thamani ya dola bilioni 2.
Hukumu hiyo inasafisha njia kwa kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya Zuma kuanza Februari 2020.
Zuma aliyekuwa madarakani tangu mwaka 200 hadi 2018, aliwahi kukata rufaa akitaka kufutwa kabisa kwa mashitaka hayo 18 ya udanganyifu, ulanguzi na utakatishaji fedha kuhusiana na mkataba huo wa ununuzi wa silaha na kampuni la Ufaransa la kutengeneza silaha la Thales katika miaka ya 1990.
Katikati ya mwezi Oktoba, mahakama kuu ya Pietmaritzburg ilitupilia mbali shauri lililoletwa mahakamani na Zuma na Thales kutaka kutosikilizwa kabisa kwa kesi hiyo. Zuma alikata rufaa tena dhidi ya shauri hilo, lakini leo mahakama hiyo ilifuta kabisa rufaa yake.