Trump alijihusisha na uchaguzi huo mwezi Oktoba kwa kusema kiongozi wa upinzani wa chama cha Labour Jeremy Corbyn hatakuwa bora kwa Uingereza na kwamba Johnson anapaswa kukubaliana na kiongozi wa chama cha Brexit nchini Uingereza Nigel Farage kufanya ushirika.
Waziri mkuu Johnson amesema hata hivyo kuwa chama chake kinaweza kutimiza matakwa na wananchi wa Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Lakini wanachama waandamizi wa chama cha Conservative wana wasi wasi kuwa Trump anaweza kuvuruga kampeni yao akiwa London, kiasi cha wiki moja tu kabla ya uchaguzi wa Desemba 12 ambao maoni ya wapiga kura yanaonesha Johnson anaweza kushinda.
