Loading...

11/29/2019

Sanamu la Zlatan Ibrahimovic lachomwa moto, kisa?


Mshambuliaji wa zamani wa timu za FC Barcelona, Inter Milan na LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amekuwa gumzo mitandaoni kufuatia jinsi ulivyopokelewa uamuzi wake wa kununua asilimia 50 ya hisa za timu ya Hammarby inayoshiriki Ligi Kuu Sweden.

Kufuatia maamuzi hayo wakati huu Zlatan akiwa kamaliza mkataba wake na klabu ya LA Galaxy ya Marekani, mashabiki wa timu yake iliyomuibua utotoni nchini kwao Sweden klabu ya Malmo wameamua kuchoma moto sanamu yake iliyokuwa imejengwa nje ya uwanja wa Malmo kwa heshima na kumuenzi mchezaji huyo.

Mashabiki hao wanamuona Zlatan ni kama msaliti kwa kwenda kununua klabu pinzani, hata hivyo timu ya Hammarby na LA Galaxy zote zilikuwa chini ya umiliki wa kampuni ya AEG Sweden kabla ya Zlatan kununua hisa Hammarby.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger