Simba SC mbioni kufungua uwanja wao wa Bunju


Katibu wa Simba SC, Anold Kashembe  imebainisha siku ambayo itazindua uwanja wake wa mazoezi uliopo Bunju Jijini Dar es Salaam.

Amesema ifikapo Desemba 7 mwaka huu utakuwa ushakamilika na kinachokwamisha kukamilika kwa uwanja huo ni kutokana na mvua zisizoeleweka kuendelea kunyesha mara kwa mara.

“Kuna mvua ambayo imenyesha hapa kati ndiyo imetibua hasa katika ule uwanja wa nyasi bandia ambapo ule udongo umevurugika, lakini upande wa nyasi asilia mambo yanakwenda vizuri.", amesema Kashembe.

Ikumbukwe Simba lianza kujenga uwanja wao wa mazoezi ambapo awali ulitarajiwa kumalizika Februari mwaka huu, lakini changamoto zilizojitokeza zikakwamisha ujenzi huo ambao sasa imetangazwa utakuwa sawa Desemba mwaka huu
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items