Singida United wahamishia kipigo kwa timu za Makete


Na Amiri kilagalila-Njombe

Timu ya Singida United imefanikiwa kupata ushindi katika timu mbili zilizopo wilayani Makete mkoani Njombe kwenye michezo ya kirafiki iliyochezwa mfululizo wilayani humo wakati ikiendelea kujifua zaidi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya timu ya Azam FC hapo baadaye.

Miongoni mwa timu zilizokutana na Singida United ni pamoja na Ujuni FC iliyopo kata ya Kitulo mchezo uliochezwa Novemba 26 na Singida United kuiadhibu timu hiyo mabao 3-1.

Hapo jana Novemba 27 Singida United ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wao dhidi ya timu ya Makete combine katika dimba la saba saba mjini Makete.

Baadhi ya makocha ambao timu zao zinashiriki ligi ya M.D.A Super Cup akiwemo kocha wa timu ya Ujuni amesema Singida United ni timu kubwa lakini wamefanikiwa kuonesha uwezo wao na kujengwa zaidi kuelekea ligi yao.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Richard Sanga amesema timu hizo ni miongoni mwa timu zitakazo shiriki ligi ya M.D.A super Cup chama cha maendeleo Makete, hivyo ameona vipaji vya vijana watakaoweza kufanya majaribio na kufanya vizuri katika timu kubwa nchini.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items