Thierry Henry amtabiria makubwa Kylian Mbappe


Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry anaamini Kylian Mbappe atatikisa zaidi katika kipindi cha miaka 20 inayokuja kwenye ulimwengu wa soka

Akiongea juu ya Mbappe, Henry ambaye anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa Ufaransa, alisema anafikiria Mbappe atakuwa mchezaji ambaye wapenzi wa soka ulimwenguni watajadili juu yake kwa miaka mingi zaidi

Ufaransa leo itaongozwa na Kylian Mbappe kushuka dimbani kucheza dhidi ya Moldova katika mchezo ambao Ufaransa akishinda itakuwa imekata tiketi ya kufuzu moja kwa moja Michuano ya Euro 2020.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items