Wimbo wa Msanii wa Nyimbo za Injili, Ben William uitwao 'Imela' umepata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki uachiwe hewani.
Ni wimbo ulinakishiwa na vionjo vya lafudhi kutoka lugha mbalimbali ambazo ukisikiliza unapata upako na kumsifu Mungu kwa neema na kipaji kikubwa alichoachilia kwa Ben William.
Imela wimbo uliorekodiwa katika Studio za Apex Music zilizoko Mwanza na video kuongozwa na Muungozaji aitwaye King Sabe.
Wimbo wa Imela umetoka baada ya kutoa wimbo wa Emmanuel, ambao pia ulifanya vizuri sanaaa.
Kwa Sasa unapatikana Youtube Akaunti ya Ben William na Mitandao mingine. Pata nafasi ya kuutazama kwenye Channel yake.