Wanafunzi 71 wagundulika na ujauzito kuanzia Januari -Novemba 2019



Na Adelina Kapaya, katavi.

Takribani wanafunzi 71  Mkoa wa katavi wamegundulika na ujauzito kuanzia Januari -Novemba 2019

Takwimu hizo zimetolewa na Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Katavi huku makosa ya ubakaji yakiwa 74 na makosa 9 yakiwa ni ulawitiwa.

Ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya watoto na wanawake Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa katavi inatoa Elimu kwa makundi mbalimbali ili kupunguza ukatili na kutetea haki za wanawake

Mkoa wa Katavi umekua na changamoto ya Watoto kuozeshwa katika umri mdogo  kuanzia umri wa miaka 11 sababu kubwa ikiwa ni wazazi kutojua umuhimu wa kumpeleka mtoto wa kike shuleni

Kutokana na hali hio  imepelekea idadi kubwa ya mimba za utotoni mkoani humo na kusababisha madhara makubwa kwa wahanga ikiwemo kupoteza maisha

Dawati la jinsia na watoto limekuwa na changamoto kubwa kuhakikisha wanatokomeza mimba za utotoni  kutokana na sheria  inayomruhusu mtu kuolewa akiwa na miaka 14 endapo sio  mwanafunzi na kwa ridhaa ya wazazi wake.

Kumekua na aína mbalimbali za ukatili ikiwa ni ukatili wa kingona,kiuchumi ,kimwili na kiakili. Mkoa wa katavi ameathirika zaidi na ukatili wa kingono.

Licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya ukatili Dawati la jinsia na Watoto kupitia uongozi wake wamejipanga kuhakikisha wanatokomeza ukatiri kwa kutoa Elimu kwa jamii.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items