Shilingi 62 milioni za malipo ya wakulima wa korosho zarejeshwa CBT



Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Takribani shilingi 62,000,000 za wakulima wa korosho katika wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale zimerejeshwa bodi ya korosho baada ya wakulima kukosea kujaza taarifa.

Hayo yamebainishwa na meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Jahida Hassan alipokuwa anaeleza mwenendo wa ununuzi na uuzaji korosho kwa msimu wa 2019/2020. Wakati wa mnada wa nne kwa msimu huu katika chama hicho cha RUNALI.

Jahida alisema ukoseaji wa ujazaji taarifa uliofanywa na baadhi ya wakulima wa zao hilo umesababisha takribani shilingi 62,000,000 kurejeshwa bodi ya kurosho.

Alisema kumekuwa na changamoto za ujazaji taarifa unaosababisha taarifa za baadhi ya wakulima kutofautiana. Hali inayosababisha washindwe kulipwa, na fedha hizo kurejeshwa CBT.

'' Fedha hizo zilizorejeshwa ni za malipo ya korosho za wakulima zilizouzwa katika mnada wa kwanza na wapili. Katika malipo ya mnada wa kwanza zilirejeshwa shilingi milioni kumi na mbili. Malipo ya mnada wa pili shilingi milioni hamsini,'' alisema Jahida.

Mbali na hayo meneja huyo wa RUNALI alisema jumla ya shilingi takribani shilingi 6.00 bilioni zimetumika kuwalipa wakulima ambao korosho zao ziliuzwa katika mnada wa kwanza na wa pili.

Alibainisha kwamba malipo ya korosho zilizouzwa katika mnada wa kwanza yalikuwa takribani shilingi bilioni moja. Ambapo shilingi  bilioni tano zililipwa kwa mnada wa pili. Nakufanya jumla ya fedha walizolipwa wakulima kwa msimu huu hadi sasa ni takribani shilingi bilioni sita.

Jahida alisema mbali na pesa hizo za malipo ya korosho zilizonunuliwa katika minada miwili na kuingizwa kwenye akaunti za wakulima. Lakipi pia fedha za malipo ya korosho zilizozwa katika mnada wa tatu tayari wanunuzi wameshaingiza kwenye akaunti ya RUNALI.

'' Tayari wanunuzi wameingiza fedha za malipo ya wakulima ambao korosho zao ziliuzwa katika mnada wa tatu. Muda sio mrefu tutaingiza kwenye akaunti za wakulima,'' alibainisha Jahida.

Changamoto ya wakulima kukosea kujaza taarifa zao lilisababisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Hassan Lugwa atoe wito na kuonya kuhusu madhara ya hali hiyo.

Lugwa alitoa wito kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wawe wanashughulikia haraka changamoto za aina hiyo zinapojitokeza.

Alisema elimu na jitihada za kushughulikia changamoto vinahitajika sana. Kwani kutoshughulikia kwa wakati kunasababisha changamoto za msimu mmoja kufika msimu mwingine. Jambo ambalo sio zuri na halikubali.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items