Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amezipa wiki moja Hamashauri zote nchini kuwasilisha taarifa ofisini kwake kuhusiana na mikopo yoyote waliyoichukua kutoka katika taasisi za fedha.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais John Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kuacha kukopa katika mabenki.
Jafo amezitaka halmashauri hizo kueleza aina ya mikopo hiyo na riba zake, pia amezitaka halmashauri ambazo zimekopa na bado hazijaitumia mikopo hiyo kuirejesha mara moja.
Katika kutilia hilo msisitizo, Waziri Jafo amuaguza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha anawasimamia Wakurugenzi na makatibu Tawala wote.
