Waziri Lugola akutana na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Polisi, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Polisi, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia kwa Kailima ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Lugola alizungumza na Wajumbe hao, masuala mbalimbali ya uzalishaji mali na kuwataka kufanya kazi kwa weledi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu), akimsikiliza Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Polisi, Hilda Tegwa, alipokuwa anazungumza katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia), pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Polisi, wakati alipokuwa anawasili katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, kuzungumza na Wajumbe wa Bodi hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.