Loading...

11/10/2019

Yanga yatoa kichapo cha goli 5-0


Vijana wa Jangwani Yanga SC leo imeichapa timu ya Nanyumbu Kombain mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Dimba la Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara.

Kijana Adam Stanley amepiga 'hat-trick' huku mabao mengine yakifungwa na Mwarami Issa 'Marcelo' kwa penati pamoja na James Willison.

Timu hiyo iko ziarani mkoani Mtwara bado ina mchezo mmoja wa kirafiki wilayani Masasi ili kujiweka sawa katika kipindi hiki ambacho ligi iko mapumziko kupisha mechi za kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger