https://monetag.com/?ref_id=TTIb Yanga yatolewa kombe la shirikisho, yapigwa tena na Pyramids | Muungwana BLOG

Yanga yatolewa kombe la shirikisho, yapigwa tena na Pyramids


Klabu ya soka ya Yanga SC imetupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kufungwa mabao 3-0 na Pyramids ya nchini Misri.

Magoli ya Pyramids yamefungwa na Traore pamoja na Farou ambaye amefunga magoli mawili.

Yanga imetolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 5-1 ukiunganisha na matokeo ya mchezo uliopita ambao ulichezwa jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo Pyramids walishinda mabao 2-1.