Alichokizungumza Mbowe mbele ya Rais Magufuli


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye ni Mbunge wa Hai,Freeman Mbowe amesema kuwa amehudhuria sherehe za miaka 58 ya Uhuru kwa ulazima wa kuwepo malidhiano.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Upinzani Bungeni,ametoa kauli hiyo baada ya Kuitwa na Rais Magufuli kutoa salamu katika kusherekea Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara inayofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

"Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa ulazima wa kuwepo malidhiano, uwepo upendo kuwepo na mshikamano katika Taifa letu, nawapongeza sana Watanzaniakwa siku ya leo na namuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu Demokrasia tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano," amesema Mbowe.

"Mh. Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika na wengine wanaumia, tumia nafasi hiyo kuliweka Taifa katika hali ya utengamano nakushukuruni sana."