Loading...

12/02/2019

Ethiopia yatangaza kuzindua satalaiti yake ya kwanza

Mamlaka ya utafiti wa anga za mbali nchini Ethiopia watangaza kuzindua satalaiti yake ya kwanza Disemba 17.

MKurugenzi wa shirika la utafiti wa masuala ya anga za mbali nchini Ethiopia, Daktari  Dr. Solomon Belay  amewafahamisha wanahabari katika mahojiano aliofanya kuwa Ethiopia inajiandaa kuzindua satalaiti yake  ya kwanza ifikapo Disemba  17.

Katika mahojiano yake na  kituo cha habari cha Ethiopia ENA,  Dr. Solomon Belay amesema kuwa satalaiti hiyo itatumiwa katika miradi ya kilimo nchini humo.

Satalaiti hiyo ETRSS-1  itarushwa nchini China na kuongozwa na kundi la wataalamu waliopo mjini Addis Ababa.

Ethiopia inaingia katika orodha ya mataifa machache  barani Afrika  Kusini mwa jangwa la Sahara lenye kumiliki Satalaiti.

Mataifa barani Afrika yenye kumiliki satalaiti ni Ghana , Nigeria, Afrika Kusini , Kenya na Rwanda.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger