Ifahamu historia ya mwanamziki Britney Spears

Nikiwa nimekaa mwenyewe nikitafakari mawili matatu, kwa mbali nasikia wimbo fulani hivi mzuri unakwenda kwa jina la “I was born to make you happy”. Ni wimbo fulani hivi mzuri wa kukonga nyonyo na maskioni pia.

Ndipo naamua kuingia mtandaoni kujua ni wimbo wa nani, ndipo nagundua anaitwa Britney Spears. Historia ya msanii huyo inaanza Desemba 2, 1981 alizaliwa mwanamuziki wa Pop na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani; Britney Spears.

Alizaliwa McComb jimboni Mississippi na kukulia huko Kentwood, Louisiana. Alianza kuonekana katika majukwaa na tamthiliya za televisheni kabla ya kusaini na Jive Records mwaka 1997. Albamu zake za kwanza mbili ‘Baby One more Time’ ya mwaka 1999 na ‘Oops!....I Did It Again’ ya mwaka 2000 zilimpa mafanikio makubwa katika soko la muziki ulimwenguni.


Britney Spears amekuwa akichukuliwa ni Malkia wa Pop kutokana na mchango wake wa kuinua vijana chipukizi katika muundo huo wa muziki miaka ya 1990 hadi 2000. Mwaka 2001 alitoa albamu nyingine ‘Britney’ pia alifanya hivyo mwaka 2003 katika albamu aliyoipa jina la ‘In the Zone’  Katika Billboards 200 amekuwa namba sita hivyo kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa tatu bora kukalia nafasi hiyo katika chati.

Singo zake nyingine zilifika katika Billboard 100 ikiwamo ya"...Baby One More Time", "Womanizer", "3", "Hold It Against Me" na “S&M” Kwa kipindi cha muongo mmoja hadi miaka ya 2000 alikuwa akishikilia nafasi ya nane ya wasanii bora duniani. Pia ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri sokoni katika sanaa ya muziki.


Britney Spears ameuza kazi zake milioni 150 duniani kote, katika hizo milioni 70 nchini Marekani pekee. Mnamo mwaka 2004 alizindua manukato yake aliyoyapa jina la Elizabeth Arden Inc. ambayo yalimpa mauzo ya dola za Kimarekani milioni 1.5 kwa mwaka 2012.

Tangu kuanza kwa masuala ya mtandao kazi za Britney Spears zimetafutwa zaidi katika mtandao wa Internet kwa miaka 12 akiwa ni miongoni mwa wasanii saba ulimwenguni kote.