Na Clavery Christian, Rubondo Geita.
Waziri wa maliasili na utalii Dr. Hamisi Kigwangalla amezindua programu ya utalii wa wanafunzi ndani ya hifadhi ya taifa Rubondo yenye lengo la kuwafanya watoto wa shule kujua umuhimu wa utalii na umuhimu wa uhifadhi maliasiri na kutunza mazingira yanayowazunguka katika maeneo yao.
Awali programu hiyo ilikuwa ikifanyika katika hifadhi za Serengeti, Ruhaha na Seluhu lakini waandaaji wa program hiyo wameua kuifanya katika hifadhi ya Rubondo ili kutoa fursa kwa shule ambazo zipo karibu na hifafhi hiyo ambapo shule tatu zitanufaika na mradi huo ambapo kila shule inapata fursa ya kupeleka wanafunzi kumi na sita (16) ambao wataweza kutembelea hifadhi hiyo na kukaa kwa siku nne (4) na kuhudumiwa kama watalii wengine wa kawaida na kutembezwa katika maeneo mbalimbali ya hifadhi hiyo na kujionea wanyama na ndege wanaopatikana ndani ya hifafhi ya hiyo.
Mbali na kuzindua programu hiyo na kukabidhi vyeti kwa washiriki waziri Kigwangala ametembelea maeneo mbali mbali ya hifadhi ya taifa Rubondo ndani ya ziwa victoria na kufanya utalii wa kuvua samaki yaani (sport fishing) na kutembelea maeneo yenye mamba pamoja na viboko na ndege wa aina mbalimbali ambapo amefurahishwa na maisha ya wanyama hao huku akiwapongeza wahifadhi wa hifadhi ya taifa Rubondo kwa kutunza mazingira ya hifadhi hiyo vizuri na kiwataka watu wengi kuja na kujionea vivutio vinavyopatikana ndani ya hifadhi za taifa ya Rubondo.
Mh, Kigwangalla anaendelea na ziara yake leo ya kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi ya taifa ya Sanane iliyopo jijini Mwanza akiwa na timu yake ya wasanii ambapo atahitimisha ziara yake ya siku tano mara baada ya kuzindua hifadhi mpya mbili huko mkoani Kagera.