Loading...

12/01/2019

KRC Genk yachapwa, Samatta aendelea kutupia

Klabu ya KRC Genk imeendelea kusuasua katika kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu Ubelgiji kwa kuendelea kupoteza michezo.

Genk wakiwa wenyeji wa Sint-Truiden na wamepoteza nyumbani kwao kwa kufungwa magoli 2-1, Genk ndio walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa Mbwana Samatta dakik ya 9.

Mambo yalianza kubadilika dakika ya 18 Yoli alipofunga goli la kusawazisha kwa Saint Truiden, ushindi wa Truiden ukathibitishwa na Suzuki dakika ya 41 baada ya kufunga goli la ushindi, huu ni mchezo wa 7 kwa Genk kupoteza, Samatta akifunga goli lake la saba msimu huu katika Ligi Kuu.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger