Liverpool yashindikana Uingereza

Beki Virgil van Dijk akishangilia baada ya kuifungia Liverpool mabao mawili dakika za 18 na 24 mara zote akiimalizia kazi nzuri za Trent Alexander-Arnold katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Bao la Brighton limefungwa na Lewis Dunk dakika ya 79 katika mchezo ambao kipa wa Liverpool, Alisson alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76 kwa kudakia mpira nje ya eneo lake.