F Watuhumiwa 20 wa kigeni wa kundi la IS washikiliwa Istanbul | Muungwana BLOG

Watuhumiwa 20 wa kigeni wa kundi la IS washikiliwa Istanbul


Shirika la habari la Uturuki Anadolu limeripoti kuwa, polisi wanawashikilia wageni 20 na raia mmoja wa Uturuki huko Istanbul kwa kushukiwa kuhusiana na kundi la IS.

Polisi wa nchi hiyo imefanya operesheni kwenye maeneo 48 kote nchini ili kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaaminika kupanga mashambulizi ya kigaidi.

Hata hivyo Polisi bado wanafanya uchunguzi ili kubaini wenyeji wa watuhumiwa hao wageni ambao hadi sasa hawajajulikana.