Zaidi ya nchi Nne kukutana Manyara kwenye Maonyesho ya 14 ya Bidhaa za Viwanda



Na John Walter-Manyara.

Ili kufikia Malengo na kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo na ufugaji,Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo mkoa wa Manyara limeandaa Maonyesho ya 14 ya kanda ya kaskazini yakishikirikisha mikoa ya Manyara,Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Maonesho hayo yanayoandaliwa kwa ushirikiano na ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Manyara yatafanyika Uwanja wa Kwaraa mjini Babati yakilenga kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na Mifugo katika ulimwengu wa Teknolojia.

Akitoa taarifa hiyo kwenye kikao cha kamati ya ushauri,mipango,utawala na maendeleo ya mkoa wa Manyara Meneja wa SIDO Manyara Abel Mapunda,amesema kutakuwa na Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini.

Amesema maonesho haya yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni zaidi ya mia nne (400)  kutoka Tanzania,Kenya,Uganda,Zimbabwe,Msumbiji,Malawi,Zambia,Burundi,Rwanda  ili kuonesha teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Kauli mbiuu ya Maonesho hayo ni, Teknolojia bora kwa viwanda vidogo na vya kati, ni nguzo ya uchumia  kwa endelevu.

Mapunda  ametoa wito kwa watu wa kanda ya Kaskazini hasa waliopo Babati na wilaya zingine za mkoa wa Manyara, kwenda kutembelea ili kuona na kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini.

Amesisitiza kuwa katika maonesho haya taasisi mbalimbali zitakuwepo ili kutoa huduma ikiwepo Taasisi ya usajili (BRELA) na Taasisi za kifedha na shirika la viwango Tanzania (TBS).