Australia: Ndege ya wazimamoto yaanguka, yauwa watatu

Wamarekani watatu waliokuwa wakishiriki katika sughuli za kuuzima moto wa msituni nchini Australia, wameuawa baada ya ndege waliyokuwemo kuanguka katika eneo la milima.

Maafisa wamesema ndege aina ya Hercules C-130 waliyokuwa wakiitumia kuuzima moto ilianguka na na kuripuka.

Ingawa chanzo halisi cha ajali hiyo hakijafahamika, Kamishna wa huduma za zimamoto katika jimbo la New South Wales Shane Fitzsimmons amesema upepo unaovuma kwa kasi katika ukanda huo umekuwa tatizo kubwa kwa ndege wanazozitumia.

Baada ya siku chache za hali ya hewa yenye ubaridi na mvua, joto kali na upepo wenye kasi kubwa vimerejea na kuzusha tena hali ya dharura katika janga la moto wa msituni linaloikumba Australia. Hadi sasa watu 32 wamepoteza maisha kutokana na moto huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi