Loading...

Jan 23, 2020

Breaking News: Waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola ajiuzuru


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kutokana na sababu mbalimbali.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa nyumba 12 za Askari Magereza kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kulikuwa na mkataba ambao ni wa ajabu.

Rais Magufuli amesema kuwa "ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"

''Mhe. Kangi Lugola nilitegemea barua yake ya kujiuzulu leo angetakiwa asiwepo hapa, Watu wamesaini mradi wa hovyo ambao hata Bunge haujui ni mambo ya hovyo watu walikuwa wanalipwa sitting allowance ya dola mia 800, Kangi Lugola pamoja na mwili wake ni Mwanafunzi wangu nimemfundisha Sengerema Secondary lakini kwa hili hapana, Commissioner Thobias Andengenye kwa hili pia Hapana''.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger