Bulaya achaguliwa kumrithi Tundu Lissu Bungeni

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemteua Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni., akichukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye alivuliwa ubunge mwaka jana.

Uteuzi huo umekuja baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kujiuzulu nafasi hiyo akidai kuwiwa vigumu kufanya majukumu yake katika nafasi hiyo kutokana na kutotambulishwa popote ikiwamo Ofisi ya Bunge.

Spika Job Ndugai leo amemtangaza Bulaya akibainisha kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe.
Mpya zaidi Nzee zaidi