China yaondolewa shutuma za kufanya hila za kifedha

Wakati Marekani na China zikielekea kutia saini makubaliano ya kumaliza mvutano wa kibiashara, wizara ya fedha mjini Washington imeondoa shutuma zake dhidi ya China, kwamba inafanya hila katika kupunguza thamani ya sarafu yake, Yuan.

Shutuma hizo ziliwekwa mwezi Agosti mwaka jana, baada ya China kupunguza thamani ya Yuan, ili kurahisisha mauzo ya bidhaa zake kwenye soko la kimataifa.

Wizara hiyo ya fedha ya Marekani, imesema hivi sasa China imekubali kuacha hizo hizo, katika vigezo vinavyoweza kuhakikiwa.

Hatua hii ni ishara nyingine kwamba mzozo wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili zinazoongoza kiuchumi duniani, ambao umekuwepo kwa muda wa miaka miwili, umeanza kupungua makali.