Halmashauri ya Tarime Mjini wapitisha Bajeti ya shilingi Bilioni 2

Na Timothy Itembe Mara.

Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara jana wamepitisha Rasimu ya Bajeti shilingi 25341898627 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Akisoma taarifa mbele ya Baraza la halmashauri hiyo Afisa Mipango,Braiton Garigo alisema kuwa mpango wa Bajeti umezingatia vipaumbele mbalimbali vya kisekta.

“Mpango na Bajeti ya halmashauri ya Mji wa Tarime kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imezingatia vipaumbele mbalimbali vya kisekta kama ifuatavyo kuimarisha maswala ya utawala Bora uendelezaji wa watumishi na mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya kata na mitaa”alisema Garigo.

Garigo aliongeza kuwa halmashauri ya Mji wa Tarime inaomba kuidhinishiwa na kutumia jumla ya shilingi 5105554897 kama fedha za maendeleo kati ya fedha hizo jumla ya shilingi 456484406 kutokana na 40% ya vyanzo vya ndani shilingi 4649070491 ni fedha kutoka serikali kuu na wahisani mbalimbali wa maendeleo.

Ofisa huyo aliongeza kuwa kwa mwaka 2020/2021 umbile la Bajeri ya halmashauri ya Mji wa Tarime inatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi 20527932601 mwaka 2019/2020 hadi shilingi 25345487502 sawa na ongezeko la 23.5% ambapo wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani utaongezeka kutoka 1249643870 kwa mwaka 2019/2020 hadi kufikia shilingi 1777985886 sawa na ongezeko la wasitani 42%.

Kwa upande wake diwani viti maalumu kata ya Nyandoto kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo chadema,Tekra Johanes aliitaka halmashauri hiyo kuwaruhusu  wafanyabiashara wa vibanda vinavyotarajiwa kujengwa maeneo ya Stendi ya Mabasi Kemange ambao maombi yao yalikidhi vigezo  kuruhusiwa kujenga ili kuongeza makusanyo   katika chanzo hicho.

Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo Khamis Nyanswi Ndera aliwapongeza madiwani kwa kupitisha Bajeti na kuwaomba watumishi kusimamia Bajeti ili kuwaletea wananchi maendeleo kwaniwao mwaka huu  wanaenda kutoka ndani ya halmashauri na kuachia madiwani wapya watakaokuwa wamechaguliwa kupitia  uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2020.