Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amjulia hali Waziri mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim anayepatiwa matibabu jijini Dar es Salaam .
Mhe. Rais ametoa wito kwa Watanzania kumuombea Dkt. Salim ili apone kwa haraka ambapo kabla kurejeshwa Jijini Dar es salaam, Dkt. Salim alikuwa akipatiwa matibabu Nchini Uingereza.