Na Paschal Malulu-Kahama
Wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Mayila iliyopo Kata ya Nyihogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameivunja kamati ya ya shule hiyo kutokana na viongozi wa kamati hiyo akiwemo mwenyekiti kuhusishwa katika tuhuma za wizi wa mifuko 15 ya saruji.
Wakizungumza kwa hasira kali wazazi hao katika kikao cha wazazi kilichoitishwa na uongozi wa serikali ya mtaa wa Mayila wazazi hao wamesema hawana imani na kamati yote ya shule kutokana na uongozi mkubwa wa juu wa mwenyekiti kuhusishwa katika wizi huo.
Solomon Juma ambaye ni mzazi aliehudhuria kikao hicho amesema hawawezi kuendelea kuwaamini viongozi ambao katika serikali ya awamu ya tano haihitaji ujanjaujanja hivyo viongozi wote wa kamati ya shule kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo wanaivunja mara moja ili kunusuru maendeleo ya shule.
Amesema wao kama wazazi wanatambua umuhimu wa elimu kwa watoto lakini kutokana na ubadhilifu wa viongozi waliopo kwa sasa hawawezi kundelea kutoa michango ya ujenzi wa madarasa ya shule hadi watakaposomewa mapato na matumizi ya fedha zilizotolewa na Rais Magufuli shilingi milioni 5 na siku hiyo watasimika kamati mpya.
Kwa upande wake mzazi Bushir Mashilabi amesema kuna viongozi wamejenga nyumba na zimekamilika kupitia fedha hiyo iliyotolewa na Rais Magufuli na ushahidi wanao na kwa pamoja kama wazazi wamekubaliana kuivunja kamati ya shule na siku ya Jumamosi wiki hii watachagua viongozi wengine.
Amesema kabla ya kuanza kutoa michango ya kuongeza vyumba vya madarasa mengine manne ambapo shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na halmashauri imewataka kukamilisha ujenzi wa maboma ndani ya wiki nne wanahitaji kusikia jinsi ambavyo fedha ya Rais Magufuli ilivyotumika huku wakimtaka mkurugenzi wa halmashauri kuwaondoa walimu wote waliotuhumiwa na wizi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mayila Idd Said amesema anakubaliana na maamuzi ya wazazi waliyoafikia kwa pamoja na yeye anaivunja rasmi kamati hiyo na kuwataka wazazi hao kujitokeza tena siku ya Jumamosi na kufanya uchaguzi sahihi wa viongozi wa kamati ya shule ambao watakuwa waadilifu.
Nae mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya Nyihogo Isaya Masota amesema tukio la walimu kuhusishwa na wizi wa mali za shule hilo limekuwa la tatu na hivyo Kata ya Nyihogo imekuwa ikipelekewa walimu ambao sio waadilifu hivyo mkurugenzi wa halmashauri anatakiwa kuangalia suala hilo.
Amesema wote waliohusika katika wizi huo yeye akiwa kama kiongozi atahakikisha vifaa vyote vinarejeshwa huku akimwagiza mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo kufuatilia vifaa vyote ikiwemo ndoo za rangi zinarudishwa kabla ya siku ya Jumamosi kwenye kikao cha wazazi.
Ikumbukwe shule ya msingi Mayila ni mpya ambayo imefunguliwa Januari mwaka huu na Rais Magufuli aliichangia shilingi milioni tano na kuagiza kusimamiwa kwa ujenzi wa shule hiyo kwa uadilifu ambapo licha ya kamati hiyo kuvunjwa imedumu kwa muda wa siku 14 ikiwa viongozi wake walichaguliwa Januari 15, 2020.