Loading...

Jan 23, 2020

Kauli ya Lugola baada ya kutumbuliwa

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola amshukuru rais na kusema anarudi kuwa mbunge wa Kawaida "Back Bencher" na kuendelea kuipambania Serikali kwa kuchapa kazi.

Mhe. Lugola amesema hayo alipohojiwa na waandishi wa habari muda mchache baada ya kutumbuliwa na amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumteua kwa kipindi chote alichokuwa Waziri na kuwataka mawaziri wengine kuchapa kazi kwa uadilifu.

"Mh Rais ndie aliyeniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri  na ndio ameona anipumzishe kwenye Baraza lake la Mawaziri kwangu mimi ni jambo la faraja amechukua hatua nzuri zinalenga kujenga safu nzuri ya awamu ya tano na bado ntaendelea kumtumikia Mh. Rais na serikali ya awamu ya tano kwa ujumla" alisema Lugola.
.
.“Alichokisema Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni maelekezo kwahiyo nitayafuata na kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais.” Mbunge Kangi Lugola akizungumza na Waandishi Ukonga.KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger