Loading...

1/13/2020

Kizimbani kwa kujifanya marehemu ili apewe mafao yake

George Mbuga, Mkazi wa Urambo Mkoani Tabora amefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi baada ya kujisingizia amefariki Dunia ili alipwe mafao yake kwa mkupuo.

Mbuga baada ya kustaafu alipaswa kulipwa fedha kwa awamu tano tofauti lakini alitumia njia ya mkato na kula njama na wenzake akiwemo Mtumishi wa NSSF na kujifanya amefariki.

Mbuga na wenzake wanne wanashtakiwa kwa makosa manane likiwemo la kuandikisha tukio la kifo kutoka Ofisi ya Kitongoji na kuzipeleka Document kwa Msajili wa Vizazi na Vifo wakiambatanisha na muhtasari feki wa kikao cha Ndugu wa Marehemu huyo feki.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger