Manara amvaa tena Nugaz "Misitu na wanyama wamekumiss bro!''

Kama kawaida yake!! Baada ya kuona msemaji mwenzake kutoka Yanga, Antonio Nugaz, akichapia kwa kusema kuwa Yanga ikishinda mechi tatu itakuwa na alama sita badala ya tisa, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameandika hiki kuhusiana na Nugaz katika mtandao wake wa Instagram.

Kupitia akaunt yake ya instagram Manara ameandika hivi;

Another Boko from mtu yule yule wa Clean Sheet
Kutokujua kama Mechi tatu ni points Tisa na sio Sita ni Uzuzu wa kutofahamu kanuni na kwa Msemaji kutojua hilo ni kuvamia fani, hebu kila mtu arudi ktk jambo lake, Misitu na Wanyama wamekumiss bro, huku unapuyanga tu kila siku.