Marcos Rojo aikimbia Man United arejea Argentina

Klabu ya Estudiantes inayoshiriki ligi ya Argentina imethibitisha kumsajili beki wa klabu ya Manchester United Marcos Rojo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Rojo mwenye miaka 29 anarejea kwenye klabu ambayo alianzia kucheza soka, hakucheza kwenye kikosi cha kwanza Man United tangia mwezi Novemba na pia alikosa kujiunga na klabu ya Everton siku ya mwisho ya usajili wa mwezi Agosti 2019.