Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amesema kutokana na ukosefu wa usafiri katika Gereza la Ulanga Mkoani Morogoro, Askari wamekuwa wakitumia Bodaboda kuwasafirisha Mahabusu kwenda Mahakamani .
Hoja hiyo ameitoa wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni na kujibiwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani.
Swali: Mh. Spika mwaka wa tano sasa gereza la Ulanga mahabusu wanabebwa na bodaboda kupelekwa mahakamani hii ni hatari sana kwa mahabusu kutoroka mh spika naomba kuuliza swali la nyongeza lini serikali itaamua kupeleka gari magereza ya Ulanga?
Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema watatatua changamoto ya ukosefu wa Magari kadri yatakapopatikana na kwamba yakipatikana watapeleka katika Gereza la Ulanga.