Rais Erdogan na Putin wazindua mradi wa gesi wa TurkStream

Marais Recep Tayyipp Erdogan wa Uturuki na Vladimir Putin wa Urusi wamezindua bomba la gesi asilia la TurkStream huku wakimwagiana sifa za mahusiano binafsi baina yao na ushirikiano wa mataifa yao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema mradi huo ni muhimu sio tu kwa Uturuki na Urusi bali pia utasaidia kuimarisha usalama kwenye sekta ya nishati barani Ulaya.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameuelezea mradi huo kuwa wenye umuhimu wa kihistoria akisema utawezesha kusafirisha gesi ya kiasi cha mita bilioni 15.75 za ujazo hadi Uturuki.

Rais Erdogan na Putin waliungana na rais wa Serbia Aleksandar Vucic na waziri mkuu wa Bulgaria Boyko Borisov kuuzindua mradi huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items