Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za mabalozi

Leo january, 28 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi wateule tisa walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao nchini humo.

Mkuu huyo wa nchi amepokea hati hizo leo Jumanne Januari 28, 2020 katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salam ambapo Mabalozi wateule waliowasilisha hati zao na kupokelewa.

Mabalozi hao  ni pamoja na Maria Amelia Mario De Paiva ambaye ni Balozi wa Ureno nchini, Douglas Foo Peow Yong ambaye anakuwa Balozi wa Singapore nchini na Balozi wa Ufilipino nchini, Alex G. Chua  Balozi wa Jamaica nchini, Angela Veronica Comfort, Christian Fellner anayekuwa Balozi wa Austria nchini na Fransisca Ashiete Odunton anayekuwa Balozi mteule wa Ghana nchini, Jesus Agustin Manzanila Puppo anayewakilisha Venezuela nchini, Balozi wa Djibouti nchini, Yacin elmi Bouh na Balozi wa Israel nchini, Oded Joseph.

Baada ya kuwasilisha hati hizo, kila balozi alifanya mazungumzo na Rais Magufuli wakijadili kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi zao.
Mpya zaidi Nzee zaidi