Spika wa Bunge, Job Ndugai amezungumzia hali ya mafuriko mkoani Lindi na kutaka ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) kuchukua hatua katika kusaidia waathirika wa mafuriko hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu nane hadi sasa.
“Ni kweli mvua inanyesha karibu kila mahali nchi nzima lakini kwa taarifa tulizo nazo hivi sasa ni kwamba katika Mkoa wa Lindi katika jimbo la Waziri Mkuu kule Luangwa kuna mafuriko kwahiyo tunakuomba sana Waziri wa nchi uweze kuona hali hiyo,” – Spika wa Bunge, Job Ndugai
Licha ya Watu wanne kufariki Wilayani Ruangwa, Lindi, zaidi ya Wananchi 20 wamelazimika kukaa juu ya miti kwa saa kadhaa ili kujikinga na mafuriko baada ya maji kuzingira makazi yao katika Kijii cha Nambiranje na Vijiji jirani.