Tamasha la KAN Festival kupamba moto January 22 hadi 25 mwaka huu



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Kituo cha Mafunzo ya Uongozi  ambacho ni cha Ushirikiano wa Denmark na Tanzania  (MS-TCDC)  kwa kushirikiana  na wasanii pamoja na  watu  mashuhuri  kimeandaa tamasha  la sanaa na Maarifa   linalojulikana kama Kan Festival litakalo fanyika eneo la Usa River katika Mkoa wa Arusha.

Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa mara ya pili lina kauli mbiu isemayo “Maendeleo ni watu si vitu) , kauli aliyowahi kuitamka Baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mkurugenzi wa sanaa katika Tamasha hilo Dave  Ojay , litafanyika kuanzia tarehe 22-25 Januari 2020, tamasha hili litakua ni fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka mataifa takribani saba ya Afrika ambao hawajawahi kukutana wataleta  SANAA mbalimbali ikiwemo maonyesho ya sanaa, muziki,uchongaji vinyago,uchoraji katuni na sanaa nyingine nyingi.

“Sanaa ina nguvu kubwa ya kuzungumza na watu ,vijana waje wajifunze wajue historia ,wajadili masuala ya maendeleo ya watu na sio vitu ,pia kuhimiza vijana kujadili maendeleo ya Afrika”  Anaeleza Dave

Mkurugenzi wa Programu katika kituo cha MSTDC ,Sara Ezra Teri  hi limelenga katika kusaidia kubadilishana ujuzi mbalimbali ikiwemo sanaa pia kuwaelimisha vijana , pia jinsi ya kuzikabili changamoto mbalimbali ikiwemo mimba za  utoto,ukosefu wa ajira,rushwa na ufisadi.