Na Amiri kilagalila, Njombe.
Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ametoa siku tatu kufanyika kwa ukaguzi kiwanda cha maziwa Njombe kupitia wakaguzi wa ndani badala ya kusubiri CAG au COHASCO huku akiagiza wote waliohusika kukihujumu kiwanda hicho kuzirejesha fedha za wafugaji huku wahalifu watakaopatikana kufikishwa mahakamani
Waziri mpina ametoa agizo hilo akiwa mkoani Njombe wakati alipozulu kiwandani hapo na kupokea malalamiko mbalimbali toka kwa wafugaji wanaodai kiwanda hicho fedha za maziwa takribani milioni 100 pasina mafanikio kwa muda mrefu sasa.
Awali wafugaji mbalimbali akiwemo Izack Msalilwa,Hezron Njiuka na Athanas Litungulu wamejitokeza mbele ya waziri mpina na kupaza sauti zao huku wakitaka serikali kuingilia kati mgogoro wao unaowafanya kushindwa kuwapeleka watoto shule na kulazimika kuanza kuuza maziwa yao nje ya kiwanda chao kutokana na kiwanda hicho kuwacheleweshea malipo.
“Nilitegemea kuja kupata majibu ya kuridhisha nafsi yangu,sisi wengine tulikuwa watumishi tukaweza kwenye uchumi wa Ng’ombe lakini nako tunaanguka,swala la biashara ya maziwa kwa kweli ni kilio kikubwa sana tunaomba waziri kwa ridhaa yako ikiwezekana kiwanda kibinfsishwe kwa mtu mwingine atakayeweza kufanya kazi na sisi”alisema Melitha Mlowe mmoja wa wafugaji
Baada ya kupokea malalamiko hayo waziri mpina ndipo akasimama na kutoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kutoa siku tatu za ukaguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na hatia za kufifisha kiwanda cha maziwa njombe.
“Mimi nasema kiungwana wale wenzetu ambao tuliwapa dhamana na waka fanya haya,kiungwana wabebe hizo burungutu za hela wampelekee mkuu wa mkoa ofisini na sisi tutaondoa shtaka hatutakuwa na kesi,wasipofanya hivyo ukaguzi siku tatu taarifa itatoka,waarifu wote watakaobainika mahakamani la sivyo wawe wamerejesha fedha za wananchi”alisema waziri Mpina
Christopher Ole Sendeka ni mkuu wa mkoa wa Njombe amemhakikishia waziri huyo kwenda kutekeleza maelekezo hayo huku akisema atashughulika na kila mmoja atakayehusishwa katika sakata hilo kama alivyoanza na waliohusika kufifisha iliyokuwa benki ya wananchi Njombe Njocoba na vyama vya ushirika.
Pamoja na mgogoro huo mkubwa baina ya wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa na kiwanda hicho lakini wito umeendelea kutolewa kwa wafugaji kuto kata tamaa ya kufuga kwani serikali ipo kwa ajili ya kushughulikia kero zao.
