Urusi: Chama tawala champitisha Mishustin kuwa waziri mkuu mpya

Chama tawala nchini Urusi United Party kimempitisha kwa kauli moja Mikhail Mishustin kushika wadhifa wa waziri mkuu kabla ya bunge la nchi hiyo kupiga kura rasmi.

Bunge la urusi Duma linatarajiwa kupiga kura baadae leo. Baraza la mawaziri la Urusi lilijiuzulu hapo jana baada ya rais Vladimir Putin kupendekeza mageuzi ya katiba yenye lengo la kumwezesha kuendelea kuwa na ushawishi wa kimamlaka hata baada ya kuondoka kwenye wadhifa wa rais.

Rais Putin amemteua Mishustin kuwa waziri mkuu mpya baada ya waziri mkuu wa hapo wali Dmitry Medvedev na baraza lake lote la mawaziri kujiuzulu hapo jana.